Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akipata maelezo kuhusu mikopo ya nyumba kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Temeke na Saba saba Kidawa Masoud alipotembelea Banda hilo wakati wa ziara yake kwenye maonyesho ya 45 ya Dar es Salaam ya Biashara ya Kimataifa yenye kauli mbiu “Uchumi wa Viwanda kwa ajira na biashara endelevu” na yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kilwa.
Meneja wa Mauzo kwa wateja Binafsi (NMB Direct Sales & Support Manager) Janet Nyamko akiwafunda wanachama wa SIDO kuhusu baadhi ya huduma za Kifedha zinatolewa na NMB kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. NMB ilitowa mafunzo haya kwenye maonyesho ya 45 ya Dar es Salaam ya Biashara ya Kimataifa yenye kauli mbiu “Uchumi wa Viwanda kwa ajira na biashara endelevu” na yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kilwa.