24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Afya wa DRC ajiuzulu

Kinshasa, DRC

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),  Oly Ilunga,  amejiuzulu kwenye nafasi yake na ameeleza sababu ya kufanya hivyo ni kutoridhishwa na namna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unavyoshughulikiwa Mashariki mwa nchi hiyo ambapo amemshutumu Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi kwa kumteua mtu mwingine kuongoza kikosi kinachokabiliana na ugonjwa huo.

Jumamosi Julai 20, Rais Tshisekedi aliteua timu ikiongozwa na  Jean-Jacques Muyembe, ambaye ni Mkurugenzi wa Chuo cha Utafiti wa ‘Biomedical’  nchini humo ili kuratibu uchunguzi wa Ebola kwa niaba ya Serikali badala ya Illunga.

Illunga aliandika barua ya  kujiuzulu jana Jumatatu Julai 22, ambapo pia aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuelezea sababu iliyopelekea ajiuzulu.

“Kwa sababu ya uamuzi wa Rais Tshisekedi kuweka mikakati dhidi ya virusi vya Ebola chini ya usimamizi wake moja kwa moja. Nimejuzulu kama Waziri wa Afya siku ya Jumatatu, ilikuwa heshima kuweka utaalamu wangu na kuihudumia nchi yangu katika miaka hii miwili ya historia yetu,” aliandika Illunga.

Ujumbe alioandika Illunga katika ukurasa wake wa Twitter akiambatanisha na barua yake ya kujiuzulu.

Aidha hatua ya Illunga inakuja siku nne baada ya shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza dharura ya kiafya duniani kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC ambao umeua watu 1,700 tangu mwezi Agosti mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles