28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ummy: Watu 1,034 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha kuna ongezeko la matukio 1,034 ya ukatili wa kijinsia kutoka mwaka juzi hadi mwaka jana.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dodoma, alipokuwa akifungua kongamano la wataalamu wa maendeleo ya jamii.

Ummy alisema takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka jana  zinaonyesha kuwepo kwa matukio 14,419 ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali hapa nchini ikilinganishwa na matukio 13,457 kwa mwaka juzi.

Alisema ongezeko hilo la matukio 1,034 ni sawa na asilimia 7.7.

Ummy alisema takwimu zinaonyesha kwamba kiwango cha taifa cha ndoa za utotoni kimefikia asilimia 31.

“Nafahamu kwamba pamoja na jitihada zinazofanywa bado kuna changamoto ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto, kama kubakwa, kuajiriwa katika kazi za hatari pamoja na mila na desturi potofu.

“Ni ukweli usiopingika kuwa teknolojia ikitumika vizuri vitendo hivi vinakoma katika jamii zetu kuhusu kutoa taarifa kwa wakati,” alisema.

Ummy alisema Serikali inathamini kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa maendeleo ya jamii hapa nchini kwani zimekuwa na manufaa makubwa katika jamii.

“Niwahakikishie Serikali ya awamu ya tano inathamini nafasi ya wataalamu hawa na tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutatua changamoto hizo,” alisema.

Alisema Serikali itaendelea kutatua changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba katika maeneo mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles