29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ummy akiri kuwepo changamoto matibabu bure kwa wazee

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amekiri kuwepo changamoto katika kutekeleza sera ya matibabu bure kwa wazee , wajawazito na watoto chini ya maika mitano.

Pia amesema asilimia 15 pekee ya watanzania ndio wenye bima ya afya hivyo wapo kwenye utekelezaji wa sheria ya bima kwa wote.

Ummy ameyasema leo Januari 10, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wakati akitoa taarifa hali ya utoaji huduma za afya kwa mwaka 2023 na mikakati yake kwa 2024 mbele ya waandishi wa habari.

Amesema kuna mafanikio mengi katika utoaji wa huduma za afya lakini kumekua na changamoto nyingi ambazo zinatafutiwa ufumbuzi ikiwemo upungufu wa watumishi na mwitikio mdogo wa wananchi kujiunga na mifuko ya huduma za afya.

“Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya mafanikio tunayoyaona leo ni kazi kubwa ya Rais wetu ili kuhakikisha kila mwananchi anakua na afya njema,”amesema Ummy.

Amesema asilimia 74 ya watanzania wanapata huduma za afya katika ngazi ya msingi yaani zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya na halmashauri.

Aidha ameeleza kuwa changamoto nyingine kubwa kwa baadhi ya maeneo ya utoaji huduma za afya ni usimamizi usioridhisha kwa baadhi ya watumishi na kutaka kuwepo dawati la huduma kwa wateja katika maeneo hayo.

Amesema mwaka 2022 wagonjwa waliotibiwa kutoka nje ya nchi walikuwa jumla 5,705 hivyo kufanya idadi hiyo kuongezeka kwa asilimia 121 hadi kufikia wagonjwa 6931 Mwaka 2023

“Wagonjwa hawa walitoka katika nchi za Comoro,Malawi, Burundi, Zambia, Congo DRC, Uganda, Zimbabwe na Kenya, hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kuboresha huduma za kibobezi imeweza kuvutia wagonjwa mbalimbali kuja kupata huduma, “amesema.

Akizungumzia mikakati ya 2024 Ummy amesema wizara imejipanga kuimarisha afua za kinga ili kuwezesha wananchi kujikinga na magonjwa lakini pia kuwezesha ufumbuzi wa mapema kwa magonjwa.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza ikiwemo kuhimiza kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji, kwani asilimia kubwa ya magonjwa yanasababishwa na mfumo wa maisha,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles