23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Tax afanya mazungumzo na Balozi wa Urusi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika ofisi za Wizara Jijini Dododma leo Mei 31, 2023.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Urusi pamoja na sekta za ushirikiano zilizo katika hatua mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

Vilevile, katika mazungumzo hayo wamejadili juu ya mkutano wa Urusi – Afrika na Kongamano la Uchumi litakalofanyika Julai 2023 nchini Urusi. Kongamano hilo linatarajiwa kutoa mtazamo wa uhusiano kati ya Urusi na na nchi za Afrika.

Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles