26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 17, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Ridhiwani: Watendaji wasimamie ubora wa elimu ili kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu ili kutengeneza jamii yenye uwezo wa kushindana.

Akizungumza leo, Februari 11, 2025, katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, Waziri Ridhiwani amesema uzinduzi wa sera mpya ya elimu na mitaala iliyoboreshwa unapaswa kuleta mageuzi chanya katika sekta hiyo.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufundishia kwa wanawake na wasichana ili kuongeza wataalamu katika nyanja za Sayansi, Uhandisi na Hisabati (STEM). Wanawake wakiwezeshwa wanaweza,” amesema Waziri Ridhiwani.

Amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu inapaswa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha wanafunzi, hususan wasichana, wanahamasika kusoma masomo ya sayansi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu Msingi, Dk. Charles Mahera, amesema serikali itaendelea kuandaa walimu bora wa masomo ya sayansi ili kuwahamasisha wasichana kupenda fani hizo.

“Tanzania ina asilimia 51.7 ya wanawake. Tukihakikisha wanashiriki katika masomo haya, tutaongeza ubunifu katika teknolojia na maendeleo ya kisayansi,” amesema Dk. Mahera.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Vyuo Vikuu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema maadhimisho haya yana lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake katika nyanja za STEM, ili kuhakikisha kuna wataalamu wa kutosha katika siku zijazo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mussa Sima, amepongeza juhudi za serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vya kati wanapata mikopo, akibainisha kuwa zaidi ya 250 wameshapewa mikopo na wengine 700 wanatarajiwa kunufaika mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles