Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Balozi. Dk. Pindi Chana amewataka wadau wa chaneli ya utalii Tanzania Safari, kuhakikisha wanatanua wigo wa vipindi vya utalii viweze kuonekana katika mitandao ya kijamii.
Waziri Dk. Pindi alitoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa chaneli hiyo na Manaibu Mawaziri kwa lengo la kujadili mikakati na maboresho ya channeli ili kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake.
Alisema kwamba baada ya uzinduzi wa Chaneli hiyo uliofanywa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Desemba, 2018 iliundwa kamati ya watendaji wa wizara kujadili na kutoa mapendekezo yatakayoboresha uendeshaji wake kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kimataifa.
“Moja ya mapendekezo ilikuwa ni kuhakikisha inapatikana katika visimbuzi vyote na majukwaa mengine nchini na hapa kuna wataalamu mtatuambia hii haitoshi tuweke na kwenye simu, mitandao ya kijamii ndiyo maana kikao cha leo kina wabobezi hivyo ni lazima tufikiri nje ya boksi kama tunazungumzia utalii siyo lazima mtu afike nyumbani ndipo awashe luninga yake zionekane hata katika vyombo vya usafiri,” amesema Pindi.
Kuhusu athahari ya UVIKO -19 katika sekta ya utalii Pindi alisema pato linalotokana na utalii lilishuka kutoka dola za Kimarekani Bilioni 2.532 mwaka 2019 hadi Sh Bilioni 1.107 mwaka 2021 lakini bado inatajwa kama sekta muhimu kwa uchumi wa Nchi.
Hata hivyo Waziri Pindi alibainisha kwamba chaneli hiyo inapaswa kuwa endelevu na vipindi vinavyoandaliwa viwe vyenye ushawishi kwa wananchi kuvutiwa kutembelea vivutio vilivyopo nchini hata mataifa ya nje kutembelea vivutio hivyo.
“Vivile kikao hiki kitoe mapendekezo ya namna ya kupata fedha za dharula kwa jili ya kushughulikia uandaaji wa vipindi vipya na kuweka mikakati ya kuhakikisha uendelevu wa chaneli hii na kamati ya Waziri Mkuu ilikutana Desemba 27, 2018 kuweka mikakati ya uendelevu wa chaneli ikiwemo ubora unaozingatia viwango vya kimataifa, uhitaji wa mafunzo, upatikanaji wa vifaa vya kisasa na kuwezesha chaneli kupatikana katika majukwaa yote,” amesisitiza Pindi.
Alihitimisha kwa kusema masuala ya utalii ni mtambuka yanayoshirikisha sekta mbalimbali kama sekta ya utalii, sekta ya uchukuzi, sekta ya habari na mawasiliano na sekta ya fedha hivyo kama wasimamizi wa sera katika Wizara husika ipo haja ya kuifahamu chaneli hiyo, lengo la kuanzishwa na umuhimu wake kwa sekta ya utaliii na uchumi kwa Nchi.
Akieleza mapendekezo yaliyofikiwa na wataalamu wa sekta hiyo mara baada ya kikao Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya alieleza maazimio yaliyofikiwa kwamba ni pamoja na Mawaziri kuendelea kupewa nafasi ya kuwasilisha mawazo yao, wanaochangia kwa kujitolea kuwezesha chaneli watambuliwe na kila taasisi kuweka utaratibu utakaowezesha uchangiaji wa Safari Chaneli.
Aidha Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji (TBC), Dk. Ayoub Ryoba akaeleza mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa chaneli hiyo ambayo ni ununuzi na ufungaji wa mitambo ya kidigitali, kurusha matangazo kote Duniani, kurushwa vipindi vyake kupitia visimbuzi vyote nchini, kuboresha vifaa, kutoa elimu ya utalii kwa watanzania kuptia vivutio vya kiutamaduni, hifadhi za wanyama na utalii wa Ikolojia.
PIC 3
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akifafanua jambo katika kikao hicho cha wadau wa channeli ya utalii Tanzania Safari Channel na Manaibu Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre Machi 14, 2022 Jijini Dodoma.
PIC