30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ndalichako akagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Wazara jijini Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua maendeleo ya awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi yake unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na katibu Mkuu katika ofisi hiyo pamoja na Wakurungenzi wa Idara, Vitengo na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma Machi 21, 2022.

Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Ndalichako amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi kwa Mkandarasi SUMA JKT ili kuendana na ratiba iliyotolewa na Serikali kukamilisha ujenzi huo.

“Ni dhamira ya Serikali kuona majengo ya ofisi yanakamilika kwa wakati ili watumishi waweze kukaa na kufanya kazi kwa pamoja hali ambayo itaongeza ufanisi wa utendaji kazi wao na utoaji wa huduma wa ofisi hiyo, hivyo ni vyema mkandarasi akaongeza jitihada katika kukamilisha ujenzi huu,” amesema Ndalichako.

Wakati huo huo Prof. Joyce Ndalichako ametaka Mkandarasi huyo kuhakikisha wanatekeleza mpango mkakati iliyojiiweka ili ujenzi wa ofisi hiyo ukamilike kwa wakati.

Kwa Upande wake, Mhandisi Ujenzi kutoka SUMA JKT, Capt. Khalfan Mturi ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mheshimiwa Waziri. Pia alieleza kuwa wamejipanga kuongeza nguvu kazi ili kufanikisha shughuli hiyo ya ujenzi.

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, Wakurungenzi wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles