29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mwinyi aridhishwa  ujenzi ofisi ya bunge

Mwandishi wetu-Dodoma

WAZIRI wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).

Mwinyi alitoa pongezi hizo   alipotembelea Ofisi ya Bunge   kukagua miradi hiyo akiwa amefuatana  na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa Suma JKT, Kanali Rajab Mabele.

“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na Suma JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai, alilipongeza Suma JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi ambayo  hadi sasa   yote inaendelea vizuri.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la ofisi ya Bunge  na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge.

Alisema kwa   ukarabati wa jengo la Ofisi ya Bunge  na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge, tayari Suma JKT wamelipwa asilimia 40 na kazi inaendelea vizuri.

“Suma JKT ni shirika ambalo tumekuwa tukifanya nalo kazi na tunaridhika na kazi zao tunatamani wapewe miradi mingi ya Serikali,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles