WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL EHUD OLMERT AACHILIWA HURU KUTOKA GEREZANI

0
630

Aliyekua Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmet, ameachiliwa huru baada kutumikia kifungo gerezani kwa miezi kadhaa adhabu aliyopewa baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.

Makosa hayo na pia lile la kujaribu kuzuia mkono wa sheria kufanya kazi yake, anasemekana aliyatenda alipokuwa Waziri wa Biashara nchini humo.

Olmert ambaye alikuwa Waziri Mkuu toka mwaka 2006 hadi 2009, ni kiongozi wa kwanza aliyehudumu cheo cha uwaziri mkuu kufungwa jela huko Israel.

Aliachiliwa huru kwa msamaha baada ya kutumikia theluthi mbili ya kifungo chake, pia kumekuwa na wasiwasi kuhusu kudhoofika kwake kiafya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here