25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu wa Ethiopia aagiza jeshi kuliokoa Taifa

ADDIS ABABA, ETHIOPIA 

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema ameamuru jeshi kutekeleza wajibu wake wa kuliokoa taifa na Umma katika jimbo la kaskazini la Tigray baada ya kukishutumu chama cha TPLF ambacho kimekuwa kikiongoza jimbo hilo tangu mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa ‘kuanzisha vita.’ 

Ahmed amekishutumu chama cha TPLF kwa kushambulia ngome ya kijeshi katika jimbo hilo. Hilo limekuja baada ya miezi kadhaa ya kuwepo kwa mvutano kati ya serikali kuu mjini Addis Ababa na mamlaka ya jimbo la Tigray. 

TPLF awali ilishutumu utawala wa Abiy kwa kutumia janga la virusi vya corona kama sababu ya kusalia madarakani baada ya utawala wake kisheria kuisha mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Serikali ya nchi hiyo mara kwa mara imekuwa ikikilaumu TPLF kusababisha vurugu nchi nzima. 

Kwa mujimu wa Taasisi inayoangalia uhuru wa mtandao, Netblocks kumekuwa na hali ya kuzimwa kwa data za mtandao na simu mapema asubuhi siku ya Jumatano jimboni Tigray. Taarifa ya Waziri Mkuu imesema kuwa “mpaka umevukwa’ na kuwa kuiokoa nchi hiyo na Umma kwa ujumla, matumizi ya nguvu yamekuwa chaguo la mwisho,” dhidi ya TPLF. 

Mwanzoni mwa wiki hii, mwenyekiti wa chama hicho Debretsion Gebremichael aliushutumu utawala wa Abiy kwa kufanya kazi na serikali ya Eritrea kuandaa mashambulizi.

TPLF ilikuwa imekuwa nguvu kubwa ya kisiasa nchini Ethiopia kwa karibu miongo mitatu mpaka Abiy alipoingia madarakani mwaka 2018.Chama hicho kimeendelea kusimamia jimbo la Tigray.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles