22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Waziri Mkuu: Mpaka wa Holili si salama

Upendo Mosha, Rombo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema mpaka wa Tanzania na Kenya wa Holili wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, hauko salama  kutokana na kuwapo kwa njia nyingi za panya ambazo wahalifu hutumia kupitisha silaha na bidhaa za magendo.

Amesema uwepo wa njia nyingi za panya katika mpaka huo zinahatarisha  usalama wa nchi zote mbili za Kenya na Tanzania na kwamba matukio ya uhalifu yanayoendelea kutokea katika baadhi ya mikoa iliyopo mipakani ni dalili mbaya kwamba mipaka haipo salama.

“Kuna viashiria vingi  vya uvunjifu wa amani katika mpka huu wa Holili na si hapa tu, bali Kuna baadhi ya mikoa iliyopo mipakani tumeshughudia matukio ya uhalifu ikiwemo utekwaji wa watoto hi ni kutokana na kuwepo kwa njia nyingi za panya  na ili tuwe salama lazima tubadilike,” amesema.

Amesema nchi hizo mbili Tanzania na Kenya ni ndugu lakini undugu huo umekuwa ukidumishwa kwa kufuata sheria za nchi husika na kila nchi ina wajibu wa kulinda usalama wake lakini kwa utamaduni huu  wa kuaminina  haziwezi kuwa salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles