32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu mgeni rasmi Mkutano Wadau wa Mkonge

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Tatu wa Wadau wa Mkonge utakaofanyika Desemba 4, mwaka huu jijini Tanga.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona katika taarifa iliyotolewa kwa umma na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa bodi hiyo Esther Mbusi, mkutano huo utawakutanisha viongozi mbalimbali wa kitaifa na Wadau wa Sekta ya Mkonge nchini.

“Napenda kuwakaribisha wakazi wa Tanga na maeneo jirani kuhudhuria kwenye Mkutano huo mkubwa wa Wadau wa Sekta ya Mkonge unaofanyika kwa mujibu wa Sheria ya Na. 2 ya Sekta ya Mkonge ya Mwaka 1997.

“Katika mkutano huo tunatarajia Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, lakini viongozi wengine watakaokuwepo kwenye ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde ambaye atamwakilisha Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, viongozi wote wa Mkoa, Waheshimiwa Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa jirani hususani ile inayolima Mkonge.

“Kama mnavyofahamu, Waziri Mkuu amekuwa mstari wa mbele na ameshika bendera ya kuhamasisha Kilimo cha Mkonge, tulianza naye tangu mwaka 2019 hadi mwaka 2021 amekuwa akija Tanga kuhimiza watu waingie kwenye Kilimo cha Mkonge kwa sababu anafahamu faida za Mkonge zao ambalo linaweza kubadilisha maisha ya Watanzania kwa muda mfupi sana, zao la kudumu la uhakika na biashara ya Mkonge ni nzuri,” amesema Kambona kwenye taarifa hiyo.

Kambona amesema mkutano huo pia ni fursa kwa Wanatanga kibiashara kwani kutakuwa na wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao watahudhuria mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya Sekta ya Mkonge nchini.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi Desemba 2, na Kikao cha Kamati Ndogo ya Maendeleo ya Zao la Mkonge inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima na Mwenyekiti Mwenza, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella utakaofanyika Desemba 3, wilayani Korogwe jijini Tanga. Kauli mbiu ya mkutano huo ni; ‘Mkonge ni biashara, wekeza sasa.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles