25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Majaliwa mgeni rasmi NMB Marathon 2021


NA MWANDISHI WETU, Mtanzania Digital


WAZIRI Mkuu , Kassim Majaliwa, amekubali kuwa Mgeni Rasmi na mshiriki wa mbio za NMB Marathon 2021, zinazotarajiwa kufanyika Septemba 25, badala ya Septemba 18 iliyotangazwa awali wakati wa uzinduzi.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, wakati wa hafla ya kutangaza wadhamini wa mbio hizo na kategori zao, iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema idadi yao imefanya kupata makusanyo ya sh. milioni 226, kati ya walizopanga kukusanya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mponzi amesema wanamshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali ombi lao la kuwa mgeni rasmi na mshiriki wa mbio hizo zenye lengo la kukusanya sh. bilioni 1 katika kipindi cha miaka minne, zitakazotumika kulipia gharama za matibabu ya akina mama wenye maradhi ya Fistula kwenye Hospitali ya CCBRT.

Mponzi amebainisha kuwa, NMB imevutiwa na uungwaji mkono si tu wa Waziri Mkuu kukubali ombi lao, bali pia kutokana na idadi kubwa ya kampuni na taasisi zilizojitokeza kudhamini, ili kufanikisha upatikanaji wa makusanyo ya kusaidia gharama za kutibu akina mama wenye maraadhi hayo.


“Tunamshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na mshiriki wa NMB Marathon chini ya kaulimbiu ya ‘Mwendo wa Upendo,’ ambazo sasa zitafanyika Septemba 25 badala ya 18 tuliyotangaza awali wakati tukizindua mbio hizi, mabadiliko yaliyolenga kuongeza muda wa usajili kama tulivyoombwa na washiriki watarajiwa.


“Shukrani za dhati pia ziwaendee kampuni na taasisi zilizoungana nasi kudhamini mbio hizi muhimu kwa ustawi wa afya za kina mama wenye Fistula nchini. Udhamini wao ni sapoti kubwa katika kukabiliana na changamoto ya maradhi hayo yanayotesa wanawake walio wengi ambao wanashindwa kumudu gharama za matibabu,” amesema Mponzi.

Akiwataja wadhamini hao, Mponzi amesema ni Kampuni za Bima za Sanlam na UAP ndio wadhamini wakuu wa kinyang’anyiro hicho kinachovuta hisia za wengi, huku Alliance Assurance wakiwa wadhamini wa kategori ya Platinum.

Kampuni nyingine na kategori zao kwenye mabano ni Jubilee Insurance, Toyota Tanzania, Britam Insurance, Coca Cola, Reliance Insurance na Aris (Gold), Jubilee Life Insurance na Metro Life Assurance (Bronze), E Fm na Tv E (Media Partner) na SGA Security na Strategies Insurance.

Mkuu wa Biasharaa na Masoko wa Kampuni ya Sanlam, Killian Nango, alishukuru kuwa sehemu ya mbio hizo zenye mlengo chanya wa kuunga mkono jitihada za Serikali na kwamba mtazamo wao juu ya ulazima wa kusapoti jamii, wamejitosa kudhamini chini ya kaulimbiu yao ya ‘Fistula Free Generation Tanzania.’

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa UAP Insurance, Nelson Rwihula, alisema kampuni yake ina wajibu mkubwa katika suala zima la ushiriki wa utatuzi wa changamoto za kijamii, hususan maradhi ya Fistula na kuishukuru NMB kwa kuwapa nafasi ya kuwa sehemu ya mbio hizo, huku akiwataka Watanzania kuunga mkono kwa kujisajili kwa wingi ili kutunisha mfuko wa matibabu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles