24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Majaliwa kuongoza kongamano la wachimbaji madini

Na Clara Matimo, Mwanza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza kongamano la wachimbaji wadogo wa Madini nchini litakalofanyika Mei 9, 2023 jijini Mwanza.

Kongamano hilo linaratibiwa na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanznaia(FEMATA)likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Amani iliyopo Tanzania Itumike Kuwa Fursa ya Kiuchumi na Tanzania Kuwa Kitovu cha Biashara ya Madini Afrika’.

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza leo Mei 8, 2023 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Dk. Steven Kiruswa baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali   yanayoojishughulisha na uuzaji wa teknolojia za kisasa za uchimbaji madini kwenye wiki ya maonesho ya madini Rock City Mall jijini Mwanza.

Amesema serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inainua sekta ya madini ikiwemo uanzishwaji wa taasissi mbalimbali zinazoshughulikia sekta hiyo ili kuwarahisishia wachimbaji wadogo wa madini kutatua changamoto zinazowakabili waweze kufanya uchimbaji wenye tija hivyo wachimbaji watumie kongamano hilo kuishauri serikali namna ya kuendeleza sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo wa kitaifa kwa kuwa ndiyo utamaduni wa watanzania.

Rais wa Femata, John Bina amesema tangu wiki ya madini inayofanyika kitaifa mkoani Mwanza ilipozinduliwa Mei 4, 2023 na Mkuu wa Mkoa huo Malima, zaidi ya mada 100 zimewasilisha na kusikilizwa lengo likiwa ni kuhakikisha wachimbaji wanaelewa zaidi sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji madini.

“Femata tunafuraha sana kwa ujio wa kiongozi wetu Mheshimiwa Waziri Mkuu hapo kesho kutuongozea kongamano letu tutatoa changamoto zetu na kuishauri serikali nini cha kufanya,” amesema Bina na kuwataka wachimbaji kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles