26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Majaliwa azindua kiwanda cha kuchakata unga wa muhogo

HADIJA OMARY, LINDI

WAKULIMA wa zao la Muhogo nchini sasa kuwa na soko la uhakika katika zao hilo baada ya kuzinduliwa kwa Kiwanda kikubwa na cha kisasa cha kuchakata unga wa mihogo kilichojengwa katika kijiji cha Mbalala Halmashauri ya wilaya ya Lindi.

Kiwanda hiko kimezinduliwa March 22 na Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa ambapo amesema viwanda vinavyojengwa nchini vitahitaji Muhogo mwingi zaidi ili kutosheleza mahitaji ya viwanda hivyo hivyo ni vyema kwa wakulima kuongeza kasi ya uzalishaji wa mihogo.

“Nidhahiri kwamba wakulima wetu wa Muhogo wanapaswa kulima kitaalamu ili kuongeza uzalishaji, Wizara ya kilimo ihakikishe wakulima wetu wanapata utaalamu wa kilimo cha kisasa,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema licha ya kiwanda hicho, Serikali imefanikiwa kupata soko la zao hilo nchini China na hadi January 2019 jumla ya Kampuni tano zinazojihusisha na biashara ya Muhogo zimeshatambulishwa nchini.

Amesema hadi kufikia Februari 2019, kampuni ya Dar Canton Ivestment imeshasafirisha tani 187 za Muhogo mkavu (Makopa) kwenda nchini China na wanatarajia kusafirisha tani 2,060 ifikapo juni 2019.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Cassava Starch Tanzania Coparation (CSCT), Christophe Gallen amesema kuwa kiwanda hicho cha muhogo kina uwezo wa kuzalisha unga wa muhogo tani moja kwa saa na tani 6,000/- kwa mwaka na kimeajili wafanyakazi zaidi ya 400 ambapo kati ya hao asilimia 97 ya wafanyakazi ni Watanzania.

Amesema pamoja na kiwanda hicho kampuni hiyo inatarajia kujenga kiwanda kingine cha kusindika chakula cha wanga lengo likiwa ni kukuza mazao yenye ubora wa hali ya juu katika mashamba makubwa yenye ufanisi yatakayosimamiwa na CSTC pamoja na kusindika mazao yote katika kiwanda kilichopo eneo la karibu.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mkumba amesema kutokana na utabili wa hali ya hewa kueleza uwepo wa mvua chache amewataka wananchi walime mazao ambayo yanastahimili ukame kama vile Mihogo, uwele na Mtama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles