27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu kukutana na Wanahisa CRDB

Eliya Mboneya, Arusha

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kukutana na wanahisa zaidi ya 29,000 wa Benki ya CRDB.

Akizungumza jijini Arusha leo Mei 15, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya benki hiyo Waziri Mkuu anatarajiwa kufungua semina ya wanahisa hao.

Amesema semina hiyo itakayoanza Mei 17, mwaka huu ikifuatiwa na mkutano mkuu Mei 18, mwaka huu utakaofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

“Niwatake wanahisa wote kushiriki semina na mkutano huo utakaopanga na kuidhinisha mikakati endelevu itakayowezesha CRDB kufanikisha malengo na kutengeneza faidi zaidi kwenu ninyi wanahisa,”amesema Nsekela.

Akizitaja ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo ni kupitisha na kusaini kumbukumbu za mkutano mkuu wa 23, kupokea na kupitisha taarifa za fedha na ripoti za Wakurugenzi.

Aidha amezitaja ajenda nyingine kuwa ni kuidhinisha taarifa maalumu ya gawio kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2018, kuchagua wajumbe wapya wa bodi, kuidhinisha uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaoukubalika kisheria kwa mwaka unaoishia Desemba 31, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles