Waziri Mkuu kujiuzulu

0
998

VALLETA, MALTA

WAZIRI Mkuu wa Malta, Joseph Muscat ameliarifu taifa lake kwamba atajiuzulu mwezi ujao, baada ya shinikizo kutoka kwa wananchi wenye hasira, wanaotaka kujua ukweli kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi,, Daphne Caruana Galizia aliyeuawa na bomu lililotegwa ndani ya gari lake mwaka juzi.

Muscat alisema amemfahamisha rais wa nchi kuwa Januari 12, 2020 atajiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha Labour, na siku zitakazofuata atauachia pia wadhifa wake wa waziri mkuu.

Kabla ya tangazo lake, watu 20,000 waliandamana mbele ya jengo la mahakama mjini Valleta, wakimtaka aondoke madarakani.

Muscat alisema katika hotuba yake kwamba ametimiza ahadi aliyoitoa kwa wananchi miaka miwili iliyopita, kwamba haki itatendeka kuhusu mauaji dhidi ya mwandishi Galizia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here