27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu kufungua mkutano wa wadau wa anga

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ambao utajadili mambo mbalimbali.

Mkutano huo utakaofanyika leo Oktoba 30,2023 jijini Dar es Salaam, moja ya mambo ya takayojadiliwa ni jinsi walivyojipanga katika kuhakikisha wanaendeleza sekta ya anga na kuwa chachu ya uchumi wa Taifa.

Akizungumzia mkutano huo jana Oktoba 29,2023 jijini, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini(TCAA), Hamza Johari wakati kusherehekea miaka 20 ya mamlaka hiyo, watafanya tathimini ya walikotoka na wanapokwenda.

“Tunatarajia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atafungua mkutano wa wadau wa anga na kusherekea miaka 20 ya TCAA na wadau wa anga kwa kujitathimini mafanikio tuliofanya na changamoto zinazowakabili,”amesema Johari.

Katika sherehe hizo, amesema TCAA ilimua kuandaa mbio zilizoitwa ‘TCAA Fun Run 2023’ za kilomita 5 na 10 ili kufanya mazoezi ya kuweka mwili vizuri kiafya.

“Tukiendelea kufanya mazoezi mara kwa mara tutaepukana na magonjwa nyemelezi ambayo yanaweza kuhatarisha afya zetu,” amesema .

Amesema jukumu lao ni kuhakikisha wadau wa anga wanafanya shughuli kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba amesema kuwa miaka 20 ya TCAA ni mageuzi ya sekta ya anga.

“Leo tulikuwa tunasherekea miaka 20 ya TCAA kwa kukimbia mbio za TCAA Fun Run 2023 kufanya mazoezi ni kuhimarisha afya ya akili zetu, “amesema Komba.

Amesema TCAA inatoa huduma kwenye viwanja vya ndege 15 nchi nzima na amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles