26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu India aionya China

NEW DELHI, INDIA 

WAZIRI Mkuu wa India, Narendra Modi ameionya tena China kutokana na  mvutano mkali wa eneo la mpakani. 

Modi amelitoa onyo hilo akitumia moja kati ya hotuba yake muhimu katika mwaka kwa kutoa ahadi ya kuliimarisha jeshi la taifa lake. 

Katika kipindi hiki cha mvutano wa kijeshi katika eneo la mpaka wa Himalaya, Modi aliiambia hadhara ya sherehe za uhuru kwamba uhuru wa India ni kitu muhimu na kwamba mahusiano na mataifa jirani yanategemea usalama na kuaminiana. 

Juni 15 kulitokea machafuko katika eneo la mpakani kati ya China na India enao  la Himalaya, kwenye mkoa wa Ladakh, ambapo askari kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha.

MGOGORO WENYEWE

India na China, mataifa mawili yenye idadi kubwa ya watu duniani , zikiwa na majeshi makubwa na silaha za kinyuklia zimekuwa zikikosoana katika jimbo la Himalaya.

Huko nyuma Jeshi la India lilisema kwamba takriban wanajeshi 20 walifariki katika makabiliano na kwamba kulikuwa na majeruhi katika upande wa China. 

Vifo hivyo vilivyotokea Juni mwaka huu vilikuwa vya kwanza katika kipindi cha miongo minne ya migogoro kuhusu mpaka unaogawanya mataifa hayo mawili.

Wakati huo vyombo vya habari vya India vilinukuu maofisa wakisema maelfu ya wanajeshi wa China waliingia kwa lazima eneo la bonde la Galwan huko Ladakh, katika eneo linalozaniwa la Kashmir.

Taarifa zinaonesha kwamba mapema Mei, vikosi vya China viliweka vyandarua na kuchimba mahandaki pamoja na kuweka vifaa vya kivita kilomita kadhaa ndani ya kile ambacho India inakichukulia kama eneo lake.

Hatua hiyo ilikuja wakati India inajenga barabara kuu ya kilomita mia kadhaa ambayo inaunganisha kambi ya jeshi iliofunguliwa tena mwaka 2008.

India ilijenga barabara kuu mamia ya kilomita ambayo imezua wasiwasi huo

China ina maoni tofauti. Inasema kwamba India ndiyo ambayo imebadilisha hali iliyokuwepo awali.

Migogoro kadhaa kati ya india na China kuhusu umiliki wa maeneo imezua vita mara tatu 1962, 1967, 1987

Majeshi yao, ambayo ni miongoni mwa makubwa zaidi duniani, yanakutana ana kwa ana katika maeneo mengi ya eneo hilo.

Kwa sasa hivi eneo hilo la mpakani linatenganishwa kwa mstari tu. Kwa sababu ya mito, maziwa na vilele vyanzo vyenye barafu, mstari unaotenganisha wanajeshi wa nchi hizo mbili unaweza kubadilika na mara nyingi vikosi vimekuwa katika hatari ya kujikuta kwenye makabiliano.

Viongozi wa China na India walifanya mkutano mwaka 2019

India na China zina mpaka wa zaidi ya kilomita 3,440 na zimekuwa na maeneo ambayo zote zimekuwa zikidai kuyamiliki.

Doria zao mipakani mara nyingi huwa zinaingiliana na matokeo yake ni makabiliano ya mara kwa mara lakini pande zote mbili zinasititiza kwamba hazijawahi kurushiana risasi katika kipindi cha miongo kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles