28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Bangladesh ashinda kwa kishindo

DHAKA, BANGLADESH

WAZIRI Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina alitangazwa kushinda kwa kishindo jana katika uchaguzi uliokumbwa na machafuko mabaya, ambao upinzani umesema ulikuwa bandia.

Katibu Mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Helal Uddin Ahmed alisema chama tawala cha Hasina, Awami League na washirika wake walipata viti 288 katika Bunge lenye viti 300, huku chama kikuu cha upinzani kikijipatia viti sita tu.

Uchaguzi huo wa juzi uliomkabidhi Hasina muhula wa nne wa uongozi ambayo ni rekodi, ulikumbwa na mapigano baina ya wafuasi wa kambi pinzani, ambayo yaliua watu 17 na kutawaliwa na tuhuma za kuchomeka kura pamoja na uwapo wa vitisho katika vituo vya kupiga kura.

Serikali ya Hasina iliendesha operesheni ya kukabiliana na upinzani, ambao ni ushirika unaoongozwa na Bangladesh National Party (BNP), ambao uliitaka tume ya uchaguzi kufuta uchaguzi huo.

“Tunataka uchaguzi mpya ufanyike chini ya Serikali isiyo na upande mapema iwezekanavyo,” Kamal Hossain, ambaye anaongoza ushirika huo wa upinzani aliwaambia wanahabari jana.

Hasina (71) amemwagiwa sifa kuchochea uchumi wa taifa hili masikini la kusini mwa Asia kipindi cha mwongo mmoja alio madarakani pamoja na kukaribisha wakimbizi wa Rohingya wanaokimbia ukandamizaji katika taifa jirani la Myanmar.

Lakini wakosoaji wanamshutumu kwa utawala wa kiimla na kukandamiza upinzani akiwamo mpinzani wake mkuu, Kiongozui wa BNP, Khaleda Zia ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 17 jela kwa ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles