28.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 27, 2022

Waziri mkuu awataka wananchi kutumia mvua kulima zaidi

Na AMON MTEGA   SONGEA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kutumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuongeza jitihada katika kilimo na kuzalisha mazao kwa wingi.

Wito huo aliutoa jana wakati akifungua Kituo cha soko la kuuzia nafaka kilichopo Kata ya Lilambo Mtaa wa Namanditi, Manispaa ya Songea ambalo litagharimu Sh  bilion 1.9.

Majaliwa ambaye yupo ziarani mkoani humo kwa siku nne alisema Ruvuma ni miongoni mwa mikoa sita ambayo imekuwa ikizalisha mahindi kwa wingi na kulisha mikoa mingine ambayo haizalishi zao hilo.

“Natoa wito kwenu wananchi mzitumie vyema mvua hizi zinazonyesha nchini kwa kuendeleza kilimo kwa wakati”alisisistiza Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu alisema serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha wakulima wanaondolewa changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo ya pembejeo na soko la kuuzia mazao hayo ambazo tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akielezea manufaa ya soko hilo, alisema kuwa kituo hicho kitasaidia kumaliza changamoto za soko la nafaka na pembejeo kwa kuwa kitakusanya wanunuzi wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Naye Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM) alisema mafanikio hayo yanatokana na jitihada za Serikali ambayo imedhamilia kwa dhati kuwainua Watanzania kiuchumi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,866FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles