26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WAZIRI MKUU ATOA NENO KWA WABUNGE

Elizabeth Hombo, Dodoma          |

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wabunge kuonyesha mshikamano na kupendana ili waendeleze jukumu la kuishauri Serikali.

Kiongozi huyo wa Serikali alitoa kauli hiyo leo katika futari aliyoiandaa kwa wabunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge.

“Nasisitiza mshikamano miongoni mwetu katika Bunge hili la Bajeti tangu lianze, tumeonyesha mshikamano na tuendeleze mshikamano huu na kupendana miongoni mwetu ili tuendelee na jukumu la kuishauri serikali,” amesema Majaliwa.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa shukrani kwa niaba ya wabunge amesema ni heshima kubwa kwani kualikwa na Waziri Mkuu si jambo ndogo.

“Kwa hiyo tujihesabie katika waliobahatika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunakushukuru na tunakuombea Mwenyezi Mungu akuongezee pale palipopungua,” amesema Spika Ndugai.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, imehudhuriwa na wabunge karibu wote wakiwamo wa upinzani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles