24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WAZIRI MKUU ATISHIA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI UJIJI


Na Editha Karlo,Kigoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ametoa siku 30 kwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kujirekebisha na kumaliza tofauti zao ndani ya siku hizo na iwapo wataendelea na malumbano yao Serikali haitosita kulivunja baraza la Madiwani.

Majaliwa aliyasema hayo jana, wakati wa mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya Kawawa eneo la Ujiji Manispaa ya Ujiji, kuwa hatua hiyo inatokana na madiwani kutumia muda mwingi wakigombana,badala ya kuwahudumia wananchi.

“Serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa kwa kuboreshewa maendeleo katika maeneo yao na si kushuhudia viongozi wakigombana kwa maslahi yao binafsi”alisema Majaliwa.

Alisema Serekali hailidhishwi na utendaji wa kazi  madiwani  hao, hivyo anawapa muda wa mwezi mmoja kujirekebisha na kumaliza tofauti zao.

“Serikali hairidhishwi na utendaji wenu na kila kinachoendelea kwenye halmashauri ninajua kila kitu  nimewapa muda wa mwezi mmoja kumaliza tofauti zenu. Nataka muendelee kufanya kazi za kuwatumikia wananchi wa manispaa hii ambao wamewachagua ili muwatatulie kero zao,si kuendeleza  changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo ya upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya”Alisema

Alisema Serekali itaboresha miundombinu ya mkoa,ikiwamo reli barabara, ujenzi wa bandari,uwanja wa ndege utakaoukuwa unatua ndege kubwa.

Alisema lengo la maboresho hayo, ni kuufanya  mko huo kuwa kitovu cha biashara kitakachounganisha nchi za,Rwanda,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi kwa kuimarisga vituo vya uwekezaji.

Naey Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliwataka wananchi kupanda zao la mchikichi kwa kuwa ni muhimu  kwa sababu Serikali imeamua kuweka nguvu zake zaidi.

“Ndugu zangu,tulikuwa na kikao cha wadau mbalimbali wa zao la mchikichiki ambapo Waziri Mkuu ndo aliongoza kikao hicho,ninawaomba tutumie fursa hii kwa kupanda miti ya michikichi kwani nikichocheo kikubwa cha maendeleo katika Mkoa wetu hasa kipindi hiki tunachoelekea uchumi wa viwanda,”alisema

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles