26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu ateta na wafanya biashara, wadau Kagera wa kahawa

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara waihakikishie Serikali kwamba watanunua kahawa yote iliyopo kwa wakulima Mkoani Kagera pamoja na kwenye vyama vya ushirika ili wakulima waweze kunufaika na zao hilo.

Ameyasema hayo leo Oktoba 6 wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara pamoja na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili Mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi Mkoani Kagera.

Aidha amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasimali za vyama hivyo na kuwahasa kutumia vizuri rasilimali hizo na endapo kutatokea na deni lolote Serikali haitousika katika ulipaji

“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya awamu ya tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhilifu huo.”amesema Majaliwa

Waziri Mkuu amewapiga marufuku wafanyabiashara wanao waibia wakulima kahawa kwa kununua kahawa mbichi zikiwa shambani

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles