WAZIRI Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, amekutwa na dhahama ya kupigwa jiwe lililorushwa na mmoja ya waandamanaji waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni.
Hayo ya kupigwa na jiwe yanakuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Waziri Trudeau alipolazimika kusitisha mkutano wa kampeni baada ya waandamanaji kuuingilia.
Kiongozi huyo alirushiwa jiwe wakati akirudi kwenye gari baada ya kumaliza kuhutubia, ikieleweka kuwa raia wa nchi hiyo wamekuwa wakiandamana kupinga hatua ya Serikali kuwalazimisha chanjo ya Corona.
Aidha, akizungumzia tukio hilo, alionekana kupuuzia tukio hilo, akisema jiwe lilimpiga begani na halina tofauti na mbegu za maboga alizorushiwa na mwanamke mmoja mwaka 2016.