29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AONYA VITA MADIWANI, WATUMISHI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa

Na MWANDISHI MAALUMU-SONGEA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa idara kwenye halmashauri za wilaya na manispaa wasaidie kutoa utaalamu badala ya kupingana na madiwani, ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Pia amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na wakuu wa idara katika utekelezaji wa miradi iliyotengwa na halmashauri.

Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, viongozi na watendaji wa Mkoa wa Ruvuma, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

“Wakuu wa idara nyie ni washauri. Tumieni taaluma zenu kutoa ushauri, semeni bila woga pale inapodidi. Ninawasihi waheshimiwa madiwani wasitumie fursa yao ya ‘kuazimia’ pale inapotokea kuna watumishi wenye msimamo,” alisema.

Akizungumzia kuhsu ukusanyaji wa mapato, Waziri Mkuu alisema Serikali iko makini kwenye matumizi kwa kila senti inayokusanywa, na akawataka watumishi hao kila mmoja aongeze mapato ya Serikali kupitia sekta aliyopo. Pia amepiga marufuku matumizi holela ya fedha za umma.

“Kuanzia leo (jana), marufuku kwa fedha iliyokusanya kwa mapato ya ndani kutumika bila utaratibu. Serikali hii haina mzaha na miradi inayotekelezwa chini ya viwango. Mtumishi ukiharibu hapa Madaba, usidhani utahamishwa, tunamalizana na wewe hapahapa.

“Wala usiombe ndugu yako akuombee uhamisho, tutakufuata huko huko,” alisisitiza.

Aliwataka watumishi wa umma wote watumie Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kutekeleza majukumu, kwani inaeleza kila kitu ambacho Serikali inatakiwa kukifanya katika kipindi cha miaka mitano.

“Zaidi ya hayo, ninawasihi kila mkurugenzi atoe nakala ya hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo aliitoa Novemba 20, 2015 wakati akizindua Bunge la 11, awape watendaji wake waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha, kwani ilitoa dira ya nini anataka kufanya katika Serikali hii,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuboresha masilahi ya watumishi na imeanza kulipa madeni yaliyolimbikizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles