30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu amshukia Kamishna wa Kazi

NA ANDREW MSECHU

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ametaka kukomeshwa  kwa urasimu unaodaiwa kusababishwa na Kamishna wa Kazi katika Wizara ya Kazi, Gabriel Malata, katika utoaji wa vibali na leseni za kazi.

Akizungumza jana katika ziara yake katika Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Majaliwa alishangazwa na taarifa za kamishna huyo ambaye ni mpya katika wiara hiyo kwamba amekuwa akikwamisha matumizi ya mfumo wa utoaji vibali hivyo kwa maelezo kuwa anahitaji kwanza namna unavyofanya kazi.

Mfumo huo hutumika kutoa vibali maalum vya kuingia nchini na kufanya kazi kwa wataalamu kutoka nje ya nchi.

“Urasimu wa aina hii ndiyo ambao tunaukataa, mtu unazuia kuendelea kutumika kwa utaratibu uliopo hadi wewe uusome kwa kisingizio cha upya wako?

“Ukishaingia wewe tayari ni sehemu yake (mfumo) na kama unaona unahitaji kujifunza unausoma mfumo wakati kazi zinaendelea. Huwezi kusema unasitisha mfumo kwa manufaa yako wakati unasababisha urasimu na kuifanya Serikali ilalamikiwe,” alisema.

“Huyo kamishna wa kazi anasomea chuo gani hadi huo mfumo usitishwe? Asitukwamishe huyo, hata kama angekuwa anasoma chuoni, huko kwenye chuo anachosomea ni mhadhiri gani ambaye anashindwa kumfundisha na kuuelewa kwa siku mbili? kisha mfumo uendelee kufanya kazi huku akiendela kukesha kujifunza? Asitukwamishe huyu…” alisisitiza.

Majaliwa alitoa maagizo hayo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe, kumweleza kuwa tangu kuteuliwa kwa kamishna huyo karibu miezi miwili sasa kumekuwa na mkwamo katika usimamizi wa mfumo huo.

Alisema kamishna huyo aliamu kuingilia mfumo huo kwa kuwa ni mgeni katika eneo hilo akiwa anatokea katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na kwamba alitaka kujiridhisha namna unavyofanya kazi ili kuwa rahisi kwake kuusimamia na kuhkikisha hautumiki kufanya udanganyifu.

Ataka wataalamu waheshimiwe

Majaliwa pia alitaka utoaji wa vibali vya wataalamu maalumu wanaokuja kwa ajili ya kufunga mitambo na mifumo ya wawekezaji viheshimiwe ambapo wataamu wanaotoka nje wanatakiwa kupewa vibali vya siku 90 kwa ajili ya kufunga mifumo hiyo na kuwaelekeza wataalamu wa ndani namna ya kuikarabati na kuiendesha.

Alisema wapo wataalamu wazuri wa uhandisi wanaofundishwa katika vyuo vikuu ya ndani ambao wanaweza kuelekezwa na kupata ujuzi wa kuhudumia mitambo na masuala ya kitaalamu hivyo hakuna sababu ya wataalamu kutoka nje kuongezewa muda bila sababu maalumu au kueneelea kuwepo nchini baada ya kumalizika siku 90.

“Kuna hili suaa la wataalamu wa nje wanapewa viza kwa ajili ya kufanya kazi nchini, muda wao unapoisha wanaendela kuwepo kinyemela halafu wanapewa vibali vya kufanya kazi wakati tunao wataalamu wahandisi wengi ambao wanaweza kupokea baada ya siku 90 na kuendelea kuendesha mitambo, hii siyo sahihi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Mwambe alimwomba Majaliwa asaidie kusimamia mabadiliko ya sheria zinazokinzana na kusambabisha usumbufu kwa utekelezaji wa majukumuya kituo hicho ili sheria iweke utaratibu wa kimfumo wa ushughulikiaji wa masuala yanayohusu wawekezaji ikiwemo sehemu ya kunzia mchakato hadi ya kumalizia.

Alisema mara nyingi kukinzana kwa sheria zinazosimamia taasisi na idara za serikali zimekuwa zikisababisha usumbufu kwa usajili na uthibitishaji wa wawekezaji hasa kutokana na kutokuwepokwa utaratibu wa nani anatakiwa aanze na nani afuate katika hatua zinazochukuliwa hadi kukamilisha usajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles