24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu aitaka NHC kushirikisha wabia wenye uwezo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha kuwa linachambua na kupitia kwa umakini wawekezaji watakaoleta maombi ya ujenzi wa miradi ya ubia na Shirika hilo ili kupata wawekezaji wenye uwezo wa kukamilisha ujenzi kwa viwango na wakati.

Amesema kuwa kupitia sera mpya ya ubia Serikali inatarajia kuona wawekezaji na shirika wanajenga ubia imara utakaosaidia ukuaji wa Sekta ya nyumba nchini ambayo ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 16, 2022) wakati akizindua sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Lengo la sera hiyo ni kuishirikisha sekta binafsi kuwekeza mitaji yake katika kujenga nyumba na majengo makubwa yenye tija kwa uchumi wa Taifa.

Amesema kuwa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika mbalimbali utaongeza kasi na kuwa chachu ya mabadiliko katika miji yetu, hivyo Serikali itashirikiana na wawekezaji kuondoa changamoto zitakazojitokeza ili azma ya kuwekeza mitaji katika sekta hiyo iweze kutimia.

“Huu ni uamuzi mzuri, unathibitisha kwa vitendo na kuunga mkono maono na maelekezo ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuvutia wawekezaji kutoka sekta binafsi kuwekeza mitaji yao ili kukuza uchumi wa nchi yetu. Serikali inafahamu kuwa ushirikishwaji wa sekta binafsi utaongeza kasi ya ujenzi na kuwa chachu ya mabadiliko katika miji yetu,” amesema.

Naye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula amesema kuwa maboresho ya sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yamelenga kuongeza ufanisi na tija kwa wabia wa Shirika hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu amesema kuwa sera hiyo imezingatia fursa za uchumi katika kipindi hiki, mafanikio na changamoto katika sera zilizopita.

“Sera hii pia itaongeza uwazi na mtu akitaka kuwezekeza kwenye miradi yetu isiwe lazima kumfahamu mtu yeyote ili uweze kupata fursa za miradi ya Shirika la Nyumba,” amesema Mchechu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles