25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

waziri mkuu afichua rushwa mpya uchaguzi

Mwandishi Wetu- Lindi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, amefichua aina mpya ya rushwa wakati taifa likijiandaa na uchaguzi mkuu Oktoba, mwaka huu, akisema wapambe wa wagombea ndiyo wachochezi  wa rushwa.

Kutokana na hali hiyo, amesema Serikali imewaagiza makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wahakikishe wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

“Watu wamezoea vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, Serikali tumeagiza kwa kamati za ulinzi na usalama zishirikiane kuhakikisha  hakuna vitendo vya rushwa katika uchaguzi na yeyote ambaye anajihusisha na rushwa asiachwe.”

Alitoa kauli hiyo juzi jioni, wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Lindi, baada ya kuwasili  uwanja wa ndege wa Nachingwea, akiwa njiani kwenda wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi.

Alisema kitendo cha kutoa na kupokea rushwa ni kosa, hivyo viongozi wa TAKUKURU hawana budi kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Aliwataka makamanda wa taasisi hizo, wilaya zote wahakikishe wanawakamata watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa, wakiwemo wapambe ambao ndiyo wachochezi wa vitendo hivyo.

Alitoa maagizo hayo ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu unakuwa huru na wa haki, kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa.

Katika hotuba yake aliyoisoma Juni 15, mwaka huu, bungeni jijini Dodoma, wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge, Majaliwa  aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi wazingatie katiba, sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi.

Alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa ujumla waendelee kulinda amani na kuendeleza mshikamano katika kipindi hiki na wakati wa uchaguzi Mkuu.

Mapema asubuhi jana,Majaliwa alikweda Zanzibar ambako alishiriki  tukio la kuvunjwa  Baraza la Wawakilishi liliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwenye ukumbi wa Baraza hilo. Pia tukio hilo lilihudhuliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles