29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

WAZIRI MBARAWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MAMLAKA YA MAJI KIGOMA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Kigoma (KUWASA), Simon Lupuga baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Mbarawa amefikia hatua hiyo baada ya malalamiko ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa mamlaka hiyo, Bonde la Mto Tanganyika na wahandisi wa maji hawatimizi majukumu katika nafasi zao kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Vile vile, Waziri Mbarawa amesema atamuagiza Katibu Mkuu kuandika barua ya uhamisho wa  Mkurugenzi huyo kurejeshwa Dar es Salaam kuanzia leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles