29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI LUKUVI KUTATUA MIGOGORO MIKOA NANE

Na Mwandishi Wetu, Arusha



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi anataraji kufanya ziara ya kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mikoa minane kuanzia leo hadi Septemba 30, mwaka huu.

Ziara hii, ni utekelezaji wa kampeni yake ya “Funguka kwa Waziri wa Ardhi” ambayo aliizindua Januari, mwaka jana yenye lengo la kuzunguka nchi nzima kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi.

Waziri Lukuvi, alisema kuanzia kesho na keshokutwa atakuwa katika wilaya ya Bunda mkoani wa Mara, kasha wilaya za Musoma na Tarime.

Kuanzia Septemba 20 hadi 30, atakuwa mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Morogoro.

“Nipo njiani nakenda Mara, ntaanzia wilayani Bunda ili kutatua mgogoro wa bibi Nyasasi Masike na kukagua kiwanja chake kama nilivyomuahidi Rais Dk. John Magufuli, alipofanya ziara wilayani Bunda na kunipigia simu moja kwa moja.

“Nimeagizwa na Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia 2020, migogoro ya ardhi iwe imepungua kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha,”alisema.

Alisema atasikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu sekta ya ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mkutano wa hadhara uliyopo ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Akiwa wilaya za Musoma na Tarime, atasikiliza na kutatua kero za wananchi zinazohusu migogoro ya ardhi papo hapo.

Alisema baada ya hapo, atakwenda mkoani Tabora na mkoani Katavi kutatua migogoro.

Akiwa mkoani Rukwa, anataraji kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa ardhi wa Shamba la Malonje lililo lenye  mgogoro wa muda mrefu.

Alisema akiwa Songwe, hasa  wilayani Tunduma atakagua na kusikilisa changamoto za mpaka wa Tanzania na Zambia.

Huko Njombe na Iringa, atatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa mikoa hiyo na akiwa Morogoro Morogoro atafika eneo la Mabwegere.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles