26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI LUKUVI ATOA UFAFANUZI WA BOMOABOMOA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa ufafanuzi kuhusu hatua ya Serikali kutekeleza bomoabomoa nchi nzima, akisema alimaanisha kwamba haitawafumbia macho watu  wanaovamia viwanja vya watu masikini.

Alitoa kauli hiyo Ikulu  Dar es Salaam jana baada ya Rais Dk Magufuli kutoa vyeti kwa kamati zilizohusika na ripoti za makinikia.

“Juzi nilikuwa Sumbawanga nikaambiwa na Mbunge wa Sumbawanga Mjini kwamba waziri hapa kwetu viongozi wote wa mkoa wameshindwa, viwanja vimepimwa watu wana hati lakini wanatokea wababe wakishirikiana na viongozi wa halmashauri wanajenga kwenye viwanja vya watu masikini ambao wana hati tayari.

“Akaniambia waziri unatoa mwongozo gani? Nikwamwambia  kwanza kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi, yale ya Sumbawanga yapo kila mahali huku Dar es Salaam ndiyo wamekubuhu.

“Kuna watu wamejipa vyeo wanajiita madalali wengine wapo ofisini kwangu wengine kwenye halmashauri, kazi yao ni kuangalia viwanja ambavyo havijaendelezwa hasa wakijua wengi ni masikini, wajane, wastaafu.

“Sasa watu matapeli na wenye nguvu wanawanyang’anya wanajenga mpaka nyumba inakwisha hana kibali cha ujenzi wala hati, haya mambo Rais tunayafahamu nimeyaona na mimi ndiyo uliniambia unayajua.

“Juzi nilichokisema Sumbawanga na ninarudia tena kwamba Serikali kupitia wizara yangu haitawafumbia macho watu wote wanaovamia viwanja vya watu wenye miliki halali hasa wale maskini.

“Watu hao wanaweza ku corrupt watu wa wizara yangu na kwenye halmashauri wakishirikina, wakajenga bila kuchukuliwa hatua hawa watu lazima wawekewe alama za x na mwishoni tutazivunja ili haki itendeke kwa wale wenye uhalali na miliki yake tutamrudishia yule masikini,”alisema Lukuvi.

Wakati akitoa ufafanuzi huo, taarifa ya juzi kupitia Kitengo cha habari cha wizara hiyo, ilimnukuu Waziri Lukuvi akiwaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini, maofisa ardhi, ujenzi na mipango miji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yaliyojengwa katika miji bila vibali na yale yanayojengwa kwa dhuluma katika viwanja vya watu wengine wenye hati miliki za ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles