20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Waziri Lugola asema CAG ni muongo

Na Maregesi Paul

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugora, amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni muongo.

Amesema kwamba taarifa iliyotolewa na CAG katika ukaguzi wake kwamba Jeshi la Polisi liliagiza sare hewa za polisi haina ukweli wowote kwa kuwa sare hizo zipo na ziko kwenye makontena katika ghala la kuu la polisi.

Ili kuthibitisha kauli yake,Waziri Kangi alisema yuko tayari kwenda kutembelea ghala hilo na kama sare hizo hazitakuwemo, uwaziri wake ana uweka rehani.

Kangi aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Pamoja na hayo,Waziri Kangi aliwataka wabunge wamuogope Mungu na kwamba wasipende kushabikia mambo yasiyokuwa na ukweli wowote na kwamba watu wasiokuwa wakweli waogopwe kama ukoma

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles