26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

WAZIRI KILIMO AWATOA HOFU WAWEKAZAJI WA NDANI

Na Upendo Mosha,Arusha

WAZIRI wa kilimo,Prof Adolf Mkenda,amewahakikishia wawekezaji wa ndani wa viwanda vya kuzalisha viuatilifu vya mazao na mifugo kuwa serikali haitanunua biadhaa hizo nje ya nchi na badala yake watanunua vya ndani ya nchini.

Prof Mkenda aliyasema hayo jana wakati akizindua kiwanda cha kuzalisha viuatilifu cha kampuni ya kimataifa ya usambazaji pembejeo nchini Cha Bajuta kilichopo,Mkoani Arusha,ambapo alisema serikali italinda viwanda vya ndani vya bidhaa hizo kwa maslahi ya wawekezaji na wajasiriamali wa ndani.

Alisema serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuagiza viuatilifu vya mazao na mifugo na kwamba iwapo wawekezaji wa ndani watazalisha bidhaa hizo kwa ubora unaotakiwa serikali haitasita kuvinunua na haita nunua nje ya nchi mpaka hapo ikithibitika kuwa vimemalizika.

“Serikali imekuwa ikitumia viuatilifu kwaajili ya korosho,pamba,kahawa na mazao mengine na fedha zinazotumika ni za wakulima na mbaya fedha hizo zinaend nje ya nchini,Kilimo chetu kinaunda ajira nje ya mipaka ya nchi….Sasa wale wanaoagiza pembejeo kutoka nje wake wazalishe hapa nyumbani serikali tutanunu”alisema Mkenda.

Waziri Mkenda alisema iwapo wawekezaji hao wataamua kuanza kuzalisha pembejeo za Kilimo na mifugo itaokoa fedha nyingi zinazoenda nje ya nchi na itapunguza gharama kwa wakulima.

“Naagiza taasisi zinazodhibiti ubora na taasisi nyingine kuchunguza ubora wa viuatilifu vinavyozalishwa hapa na kama vinaubora hatuta nunua nje kabla hatujamaliza vya ndani na maana tunaamini tukifanya hivyo pato la nchi litakuwa na kuboresha maisha ya watanzania ikiwemo wakulima.

“Tutaongeza fedha katika sekta ya Kilimo eneo la utafiti na ugani itasaidia kukipeleka Kilimo chetu katika maendeleo ya uchumi shindani sambamba na mpango wa miaka mitano wa kuboresha sekta hii tunahitaji mazao ya chakula kushuka bei sana lakini mkulima naye apate fedha na faida sana hii inawezekana kwa wakulima kulima Kilimo chenye tija eneo dogo kwa mazao mengi”alisema

Akizungumzia ujenzi wa Kiwanda hicho,alisema uwekezaji huo utaleta tija na kushogeza huduma za viuatilifu kwa wananchi na kwamba hatua hiyo inaunga mkono jitihada za serikali za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Gesso Bajuta,Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka huu na kwamba kitazalisha zaidi ya Lita milioni 4.5 kwa mwaka. Za viuatilifu.

“tutazalisha kwa wingi kiwanda kikiwa tayari kwani kwa Sasa tunaagiza zaidi ya Lita milioni Moja tu kwa mwaka Kwani viuatilifu nitakuwa vikipatikana kwa urahisi na kwa Bei nafuu kwa wakulima”alisema

Alisema licha ya kuwa kuwakopesha wakulima pembeje wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuwadai wakulima fedha na kushindwa kurejesha kutokana na hali ya msimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles