24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Kanyasu ataka wananchi wafuate sheria

Mwandishi Wetu- Dodoma

NAIBU  Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka wananchi wafuate sheria  kwa kujiepusha kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi ili kujenga uhusiano mzuri baina yao na wahifadhi.

Aliwataka wananchi kuwachukulia wahifadhi hao   kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda maliasili  kwa niaba yao.

Akizungumza na  watumishi  wa pori la akiba la Swagaswaga katika Wilaya ya Chemba  jijini Dodoma jana, Waziri  Kanyasu alisema wahifadhi wamepewa jukumu la   kulinda hifadhi za Taifa na wamekuwa  wakifanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

”Sisi ni wa moja hakuna haja ya kujengeana uhasama kati  yetu,wananchi wafuate sheria za uhifadhi  na wahifadhi fuateni sheria wakati mnapokabaliana na wananchi,” alisema.

Aliema wahifadhi wa wanyamapori na misitu wanazilinda rasilimali hizo kwa ajili wote, vitu kama mvua, hali ya hewa safi pamoja na mvua ni moja ya faida za moja kwa moja zinazopatikana kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa vizuri.

Alisema wahifadhi wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

“Sisi kama wizara tunaamini wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma tume maalumu kuchunguza na kuchukua hatua,” alisema

Alisema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

Alisema  wahifadhi ni watu muhimu saba kwa vile bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

“Kuna watu wanatamani kuona  misitu na wanyamapori wote tunawamaliza ili wapate maeneo ya malisho na kilimo, nawambieni tukithubutu kufanya hivyo huu ndo utakuwa mwisho wetu wa maisha,” alisema.

Alisema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Swagaswaga, Alex Choya  alisema  kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi za Taifa na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles