23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Jenista Mhagama aipongeza WHC, aitaka kushirikiana na taasisi nyingine

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Muhagama ameliagiza Kampuni ya Nyumba ya Watumishi Hosing (WHC) kushirikisha Taasisi za zingine za umma zinazotoa huduma muhimu kwa Jamii ili kupunguza gharama za maisha kwa wapangaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na viongozi kutoka Watumishi Housing Company (WHC), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) alipotembelea mradi huo ambao uwekezaji wake unahusisha Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa NSSF. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu.

Waziri Jenista ametoa agizo hilo Dar es Salaam, leo Jumatano Julai 7, 2021 baada ya kutembelea mradi wa nyumba 65 za WHC zilizojengwa eneo la Bunju B ambapo mbali na kuipongeza taasisi hiyo kwa kuwasaidia watumishi wa umma kupata makazi bora pia amebaini kuwapo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa barabara na shule.

Amesema mradi mkubwa kukosa huduma muhimu sio jambo zuri kwani inawapa changamoto wahitaji kwenda kutafuta huduma hizo mbali badala ya kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi.

“Niwapongeze WHC kwa mradi huu mzuri kwani nyumba ni nzuri na zinavutia binafsi nimeridhika, lakini kuna changamoto za hapa na pale ambazo nimeziona ikiwamo barabara. Hivyo niwaagoize viongozi wa WHC katika miradi mingine mikubwa inayokuja lazima tushirikishe na mamlaka zingine za kutoa huduma muhimu kama maji barabara na huduma zingine kama zahanati na shule ziwe karibu kwa sababu uhitaji unakuwa makubwa,” amesema Jenista ambaye ameonyesha kuridhishwa na nyumba hizo..

“Awali nilijua nyumba hizi bado hazina watu, lakini nimefurahi kukuta kwamba zilishakamilika na kuna watu tayari wanaishi, hivyo hili limenivutia sana na niwapongeze WHC kwa hiki mnachokifanya,” amesema Jenista.

Aidha, ameiagiza WHC kuangali mbali kwa kutenga maeneo ambayo yatakuwa muhimu kwa kujenga huduma hizo ili kuwavutia watumishi na wafanyakazi wa sekta binafsi kwenda kununua au kupanga nyumba hizo.

Upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa WHC (WHC), Dk. Fredy Msemwa, amesema watafanyia kazi maelekezo hayo lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watumishi wanaopata fursa ya kuishi kwenye nyumba hizo wanakuwa kwenye mazingira bora.

“Tumepokea changamoto kutoka kwa Waziri ambayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunashirikiana na taasisi nyingine katika kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwenye miradi inayotekelezwa na WHC , hivyo tunaahidi kufanyia kazi ushauri hu kwani lengo ji kuona watumishi na Watanzania wanaopata fursa ya kuishi kwenye nyumba hizi basi wanapata huduma muhimu,” amesema Dk. Msemwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles