27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Celina Kombani afariki dunia

kombani masikini

NA KULWA KAREDIA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani amefariki dunia.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila aliliambia MTANZANIA jana usiku kuwa Waziri Kombani alifikwa na mauti katika Hospitali ya Apollo nchini India ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu karibu wiki mbili.

“Ni kweli Waziri Kombani amefariki dunia leo jioni (jana), kwa saa za kwetu..alikuwa India kwa matibabu karibu wiki mbili hivi.

“Mimi kama kiongozi wa Bunge naweza kuthibitisha hili, unajua huyu ni kiongozi wa Serikali na wao wangeweza kusema lakini ridhika kwamba ametutoka.

“Alikuwa kwenye timu yetu ya matatibu naamini Serikali kesho
(leo), itatoa taarifa zaidi,” alisema Dk. Kashilila Kombani ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki tangu mwaka 2005, alizaliwa Juni 19,1959 mkoani Morogoro.

Alianza elimu ya msingi mwaka 1968 hadi 1975 katika Shule ya
Kwiro, baada ya hapo mwaka 1975 hadi 1978, alijiunga na Shule ya Sekondari aliposoma hadi kidato cha nne.

Mwaka 1979 hadi 1981,alijunga Shule ya Wasichana Tabora kwa ajili ya masomo ya kidato cha sita.

HISTORIA
Alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki mwaka 2005, akashinda nafasi hiyo tena mwaka 2010.

Kombani ametumikia nafasi mbalimbali serikalini enzi za uhai wake, ikiwa ni pamoja na waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI).

Kombani pia amewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, kabla ya kuhamishiwa ofisi ya rais anayeshughulikia utumishi wa umma.

ELIMU:
Alihitimu Stashahada Chuo cha Uongozi wa Maendeleo Mzumbe (IDM) mwaka 1985. mwaka 1992 hadi 1994, alihitimu Shahada ya Uzamili ya Uongozi (IDM) Aliwahi kuwa Ofisa Tawala Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Meneja wa Kiwanda cha Maturubai
Morogoro (Morogoro Canvas Mill)( 1994-1995) Mwaka 2008-2010.

Katika uchaguzi wa mwaka huu Kombani alikuwa akitetea kiti chake cha ubunge, baada ya kushinda kura za maoni cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilizofanyika Agosti mosi, mwaka huu.

Kifo hicho kimetokea ikiwa imepita wiki moja tangu kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Lushoto, Mohamed Mtoi (Chadema).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles