29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Aweso awaomba wakuu wa mikoa kushiriki kikamilifu usimamizi miradi ya maji

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amewaomba wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kushirikiana katika usimamizi wa miradi ya maji nchini.

Aweso amesema hayo katika kikao cha mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ya Tanzania Bara kinachofanyika jijini Dodoma.

Amesema Wizara ya Maji imedhamiria kuhakikisha lengo la kumtua mama ndoo ya maji linafikiwa kama lilivyoelekezwa na serikali.

“Niwaombe viongozi tushirikiane kwa dhati kuhakikisha tunaondoa changamoto zote za upatikanaji wa huduma ya majisafi. Peke yetu hatutaweza,” amesema Aweso.

Waziri huyo pia amepokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa viongozi hao wa mikoa na kuwaahidi kuyafanyia kazi likiwemo suala la kuwa na utaratibu wa wadau wa maji kukutana na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta hiyo.

“Naomba nipokee ushauri wenu wa jinsi ya kulitekeleza ili liwe endelevu, isiwe ni maelekezo ambayo yanaweza kubadilishwa na kiongozi mwingine. Liwe ni mwongozo rasmi na utamaduni ili hata kiongozi ajaye afanye hivyo hivyo,” amesema.

Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji haitakuwa kikwazo katika kufikia malengo huku akitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa ili kuimarisha usimamizi wa miradi ya maji kuwa ni pamoja na uamuzi wa kuingia makubaliano na Chuo cha Maji ili kuwatumia wahitimu wa chuo hicho katika usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles