WAZIRI AWATETEA WANAFUNZI VYUONI WANACHAMA WA CCM

0
457

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema  wanafunzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaosoma vyuo vikuu wamekuwa wakifuata taratibu katika mikutano yao tofauti na wanafunzi   wanaotokea Chama cha Demorasia na Maendeleo (Chadema).

Hayo aliyaeleza jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msingwa (Chadema).

Msigwa alidai  wanachama wa  Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Chadema  (Chaso) wanazuiwa kufanya mikutano  wakati wenzao wa CCM wakiruhusiwa.

‘’Unawezaje kusema Demokrasia tunafanya kwa kiwango kikubwa  wakati kuna upendeleo wa waziwazi  ni sawa na katika ndondi mmoja amefungwa mikono  halafu unasema upigane.

‘’Je, waziri atakuwa tayari kuliagiza Jeshi la Polisi liache upendeleo katika kutekeleza majukumu yake  ya Kupractise Demokrasia,’’ aliuliza Msigwa.

Akijibu swali hilo, Mwigulu alisema katika kufanya mikutano kuna taratibu ambazo zinatakiwa zifuatwe kabla ya kuomba kufanya mkutano wowote.

 ‘’Kuhusu mikutano taratibu zipo wazi  kama CCM wamefuata taratibu na wengine wanatakiwa kufuata taratibu zilezile  waweze kupewa mkutano.

‘’Lakini wengine kama hawajafanya utaratibu hawatapewa  na hawezi kupewa tu kwa sababu CCM walipewa  watapewa kwa kufuata utaratibu  na tumekuwa tukifanya kote.

‘’Mbona kuna sehemu nyingine Chaso hao hao wamepewa nafasi  ya kufanya mikutano kwa hiyo kinachotakiwa ni kufuata utaratibu wa kupewa mikutano hiyo,’’ alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here