22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Waziri awaasa wananchi kutoharibu mazingira  

january-makamba-e1424254098756Na Eliud Ngondo, Ileje

WAZIRI wa Muungano na Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba amewataka wananchi kujali maisha ya vizazi vijavyo kwa kutokuharibu mazingira wakati wakifanya shughuli zao za maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa jana wilayani Ileje mkoani Songwe, wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Lubanda.

Makamba aliwataka wananchi kutunza rasilmali mbalimbali walizozikuta katika mazingira yao ili kuepuka kuathiri ikolojia iliyopo, wakijali maisha yao ya wakati huu bila kujali vizazi vingine.

“Kumbukeni baada ya sisi kuondoka hapa duniani,kuna vizazi vijavyo, msije mkawa chanzo cha kufupisha maisha ya vizazi hivyo kwa kuharibu rasilimali tulizozikuta ambazo zimechangia kufikisha uhai wetu hapo tulipo” alisema Makamba.

Alisema baadhi ya shughuli za uharibifu wa rasilimali alizojionea wilayani humo, ni matumizi mabaya ya mito ambapo watu wamekuwa wakitumia vibaya pasipo kufuata sheria zilizopo.

Alisema wananchi wa milimani ambako ni vyanzo vya mito wilayani humo wamekuwa wakijichukulia maji kwa kuyachepusha na kubadilisha mwelekeo pasipo kufuata taratibu.

“Kufanya hivi kunaathiri watu wengine walio mabondeni wanaotegemea mito hiyo kwa shughuli za kila siku, hivyo kinacho takiwa ni kuwepo na utaratibu mzuri wa kuweza kuhakikisha maji hayo yanakuwa ni kwa manufaa kwa watu wote” alisema Makamba.

Alisema shughuli zinazo haribu mito ni kilimo, ufyatuaji matofali na upandaji miti usiozingatia hifadhi ya mazingira na katika kijiji cha Kalembo imekuwa ni mfano wa uharibifu huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Joseph Mkude alisema vyanzo 830 vimetunzwa na wananchi ndyio wamekuwa walinzi.

Alisema wamekuwa wakitunza vyanzo vya maji kwa kutoharibu uoto wa asili wakiwashirikisha wananchi kupitia viongozi wa vitongoji,vijiji na kata.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa kata ya Lubanda ambao ni miongoni watu wanao kuchepusha mito hiyo, walimwomba waziri kuwaonea huruma kwa vile shughuli zao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles