31.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AUAWA KWA RISASI BURUNDI

BUNJUMBURA, BURUNDI


emmanuel-niyonkuruWAZIRI wa Maji, Mazingira na Mipango wa Burundi, Emmanuel Niyonkuru amepigwa risasi na kufa jijini hapa jana, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi.

Niyonkuru (54) aliuawa usiku wa kuamkia jana, kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa kwa njia ya mtandao wa twitter na msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye.

Mauaji hayo, ambayo ni ya kwanza dhidi ya waziri wa serikali aliye madarakani tangu Burundi izame katika machafuko ya kisiasa kufuatia uamuzi tata wa Rais Pierre Nkurunziza wa kuwania urais kwa muhula wa tatu mwaka 2015, unakuja baada ya miezi kadhaa ya utulivu.

“Waziri wa maji na mazingira aliuawa na mhalifu mwenye bastola wakati akielekea nyumbani kwake huko Rohero, saa 6:45 usiku,” Nkurikiye aliandika saa nne baada ya kutokea tukio hilo.

Aliongeza kwamba mwanamke mmoja anashikiliwa kufuatia mauaji hayo.

Pia kwa njia ya Twitter, Rais Nkurunziza alituma salamu za rambi rambi kwa familia ya marehamu na Warundi akiapa kuwa wahalifu wataadhibiwa vikali.

Watu 500 wameuawa na wengine 300,000 kuikimbia nchi tangu machafuko yalipoibuka Aprili 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles