26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WAZIRI ATIMUA BODI YA SHULE KWA UBAKAJI

NAIROBI, KENYA


WAZIRI wa Elimu wa Kenya, Amina Mohamed ameivuja Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Moi, baada ya mwanafunzi kubakwa katika bweni

Hatua hiyo imekuja huku mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyopo mjini hapa, Jael Mureithi akichukua hatua ya kustaafu kama ilivyotaafiwa na Tume ya Huduma za Walimu (TSC).

Aidha, chama cha walimu na wazazi wa shule hiyo kimevunjwa huku wazazi wakipanga kukutana na mameneja wa shule waliobakia, Jumapili ijayo.

Hayo yote yametokea jana wakati Serikali ikiwachukulia hatua maofisa wa shule hiyo ambayo vyombo vya habari vya Kenya vimekuwa vikiripoti tukio la lililotokea shule hapo kwa uzito mkubwa.

Mohamed ameamuru kuvunjwa kwa timu ya ulinzi katika shule hiyo iliyopo Kaunti ya Kibra mapaka ja[p mabadiliko ya usalama yatakapokamilika.

Alisema wanafunzi, walimu, wafanyakazi na wageni wote wanaoingia shuleni lazima wakaguliwe.

Uamuzi wa mkuu wa shule kustafu mapema umekuja siku moja tu baada ya wapelelezi kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Makosa Makubwa ya Jinai na Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua sampuli za vinasaba kutoka kwa wafanyakazi wanane wa kiume, wakiwamo walimu sita kwa ajili ya uchambuzi wa alama za vidole.

Kwa mujibu wa uchunguzi wanaume hao wanaishi ndani ya shule au wanaaminika walikuwa shuleni wakati wa kitendo cha ubakaji kilipofanyika, alfajiri ya Jumamosi.

Wakati huo huo, vurumai, milio ya risasi na mabomu ya machozi yalitawala eneo la Kibra jana wakati maafisa wa polisi walipokabiliana na wakazi wanaopinga kubomolewa kwa vibanda vya biashara vilivyopo karibu na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Moi.

Polisi wameweka kambi shuleni hapo kuendelea na uchunguzi na kuondoa mazingira yoyote yanayohatarisha au kuwa maficho ya uhalifu katika shule hiyo ambayo mwaka jana pia ilikuwa vochwa vya habari katika vyombo vya habari baada ya wanafunzi wanane kufa kwa moto ulioteketeza moja ya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles