26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri ataka utafiti kuondokana na umasikini wa kipato

Mwandishi wetu

-Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kutafiti kwa kina namna wananchi wanavyoweza kuondokana na umasikini wa kipato na namna miradi ya Serikali inavyoweza kutekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya fedha kuliko ilivyo sasa.

Dk. Kijaji alitoa rai hiyo wakati akiwatunuku astashahada na shahada wahitimu 3,182 wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma wakati wa sherehe za mahafali ya 33 ya chuo hicho.

Alisema matokeo ya utafiti yataisaidia Serikali na jamii kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na umasikini wa wananchi, hususani wa vijijini na kuharakisha maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha miradi inayotekelezwa na Serikali inakuwa na tija.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Pius Mponzi, alimwahidi Dk. Kijaji kwamba wataongeza jitihada eneo la utafiti na kuhakikisha matokeo yanawafikia wananchi kwa lugha rahisi

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya alisema chuo chake kimetimiza miaka 40 tangu kianzishwe na kimepata mafanikio makubwa kwa kutoa wahitimu mahiri na wenye kukidhi mahitaji ya soko.

Alisema kuwa chuo kimeongeza idadi ya kozi kutoka moja mwaka 1980 hadi 25 mwaka huu, huku idadi ya wanachuo wanaodahiliwa nayo imeongezeka kutoka 13 mwaka huo hadi kufikia zaidi ya 11,000  mwaka huu.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles