25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ashangazwa na vipaumbele vya wakurugenzi

tizeba.Na Eliud Ngondo, Songwe

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, ameshangazwa na uchache wa maofisa kilimo wilayani Mbozi, huku wakurugenzi wakielekeza vipaumbele vyao katika sekta zisizo muhimu.

Alisema wakurugenzi wanatakiwa kuzingatia vigezo vya ajira kwa watumishi wa wilaya zao vinavyoendana na mahitaji ya wananchi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Mbozi mkoani hapa, Dk. Tizeba alisema wilaya hiyo ni maarufu kwa kilimo cha mahindi lakini anashangaa kuona watendaji hao ambao ni maofisa kilimo wakiwa ni wachache licha ya umuhimu wao.

“Wilaya ya Mbozi ina uhaba wa maofisa kilimo 125 wa vijiji ambao wangekuwa ni msaada mkubwa wa kuwaelimisha wakulima, badala yake Mkurugenzi anaweka vipaumbele kwa idara nyingine ambazo si muhimu sana kama wananchi wanavyotaka kusaidiwa na wataalamu hao,” alisema.

Alisema wakurugenzi wanatakiwa kuzingatia sana vipaumbele vya ajira kwa watumishi mara wanapoomba kwa kuwa ni mahitaji makubwa kwa wananchi kuweza kusaidiwa.

“Mfano mkurugenzi wa wilaya hii ya Mbozi anasema ameomba vibali vya kuajiri watumishi 500, lakini wengi wao ni idara ya afya na elimu wakati mahitaji ya wananchi ni kwenye kilimo kutokana na wilaya hiyo kujishughulisha zaidi na kilimo,” alisema Dk. Tizeba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Edina Mwaigomole, alisema kutokana na uhitaji mkubwa wa Wananchi, watazingatia maagizo ya waziri pamoja na kuomba kubadilishwa kwa vipaumbele vya ajira ili vijikite zaidi katika maofisa kilimo ambao wamekuwa ni uhitaji kwa wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles