23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AMPA MAAGIZO MGANGA MKUU MUHEZA

Na AMINA OMARI- MUHEZA


ummy-mwalimuWAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ametoa siku 14 kwa Mganga Mkuu  wa Wilaya ya Muheza, Dk. Mathew Mganga, kuhakikisha anapeleka daktari katika Zahanati ya Mgambo inayokabiliwa na  uhaba wa watumishi wa afya.

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo kituo hicho kilichojengwa kwa nguvu za wananchi tangu kikamilike mwaka 2014 na kuanza kutoa huduma hakijawahi kuwa na daktari.

Waziri Ummy aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.

“Pamoja na uhaba wa watumishi wa sekta hiyo, lazima vitolewe vipaumbele kwa zahanati zilizopo pembezoni na kwenye wakazi wengi ili kuwapa haki ya kupata huduma.

“DMO hii siyo haki, wananchi wamejitolea wenyewe kujenga hospitali, lakini kuwaletea watumishi pia mmeshindwa. Sasa baada ya wiki mbili, nataka kuwe na daktari hapa,” alisema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu, alichangia mifuko 100 ya saruji pamoja na mabati 50 kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa jengo la kutolea huduma ya mama na mtoto katika zahanati hiyo ya Mgambo.

“Kutokana na juhudi zinazofanyika, nimeamua kuwapatia vifaa vya ujenzi ambavyo vitasaidia kukamilisha jengo hili kwa haraka ili wananchi waweze kupata huduma bora ya afya.

“Nimeridhishwa na juhudi mlizozionyesha, hivyo nachangia mabati na mifugo ya saruji ili mkamilishe ujenzi wa jengo la kinamama na watoto ili waweze kupata huduma za afya karibu na kata badala ya kutembea umbali mrefu,” alisema mbunge hiyo.

Nao baadhi ya wananchi waliozungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, walipongeza msaada huo na kusema utaweza kuharakisha ukamilishaji wa zahanati hiyo na kuanza kutumika mapema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles