WAZIRI AMJIBU RAILA SAKATA LA MAHINDI

0
559

NAIROBI, KENYA


WAZIRI wa Ugatuzi, Festus Mwangi Kiunjuri, amemtaka kinara wa Chama cha upinzani cha ODM, Raila Odinga amkome katika kile alichotaja wito alioutoa kuwa afutwe kazi kwa sababu ya upungufu wa mahindi nchini hapa.

Amemtaka Odinga aelewe kuwa ‘sisi katika serikali hatuwezi kuchukua amri kutoka kwa mwanasiasa ambaye hana cheo kwa sasa kinachotambulika kisheria.

Amesema kuwa Odinga ni mwaniaji tu wa urais kama Mkenya mwingine yeyote aliye mtaani akimenyana na Rais Uhuru Kenyatta ambaye kwa sasa yuko madarakani.

Kiunjuri katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa moja kwa moja katika kituo cha redio amesema kuwa “mdomo wa Odinga hutoa maneno magumu kama maandishi ya kihindi”.

Amesema kuwa Odinga mwenyewe “wiki iliyopita alinukuliwa akisema kuwa hapa Kenya hakuna upungufu wa mahindi na haelewi ni kwa msingi gani ambapo serikali inaagiza mahindi kutoka mataifa ya kigeni.”

Akasema, “alituambia kuwa mahindi yamejaa kwa wingi nchini Kenya na kwamba tumepakia kwa meli baharini ili kuwahadaa Wakenya kuwa tunaagiza kutoka ng’ambo. Wiki hii sasa Odinga huyo huyo amesema kuwa hakuna mahindi hapa Kenya na tunapaswa kununua kutoka Ethiopia. Odinga wa wiki ya jana si Odinga wa wiki hii.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here