Waziri akipa maelekezo Chama cha Walimu

0
1208

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amekitaka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kusimamia na kuweka wazi mikataba yote ya miradi ya uwekezaji na vitega uchumi.

Pia, amekitaka chama hicho kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wanachama wake ili waweze kujua kinachoendelea katika chama chao.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini hapa, wakati akizungumza na wajumbe wa chama hicho katika mkutano maalumu wa kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Waziri Mhagama alisema kufuatia ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyotolewa kwa CWT, lazima chama hicho kisimamie na kuweka wazi mikataba yote ya miradi ya uwekezaji.

Pia, alikitaka kuweka wazi vitega uchumi kwa uhalisia wake pamoja na kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wanachama wake.

“Kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyotolewa kwa CWT, ninawataka sasa kusimamia na kuweka wazi mikataba yote ya miradi ya uwekezaji kwa sababu baadhi ya wanachama wenu hawajui kinachoendelea,” alisema Mhagama.

Pia, waziri huyo aliagiza uongozi wa chama hicho, kuwa na utamaduni wa kuwajibika na kusimamia vema miradi ya chama kwa manufaa ya wanachama.

Kwa upande wake, Rais wa CWT, Leah Ulaya, alisema wamejipanga kusimamia miradi yote ya chama pamoja na mikataba yote iliyoingia kati ya chama na wawekezaji ikiwamo vitega uchumi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tumejipanga kusimamia miradi yote ya chama pamoja na mikataba yote iliyoingiwa kati ya chama na wawekezaji ikiwamo vitega uchumi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini,” alisema Ulaya.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Tumaini Nyamhokya, alisema wanaendelea kufanya kazi za wanachama kwa uwazi na uwajibikaji na kwamba Tucta itaendelea kutoa ushirikiano kwa lengo la kuboresha masilahi ya watumishi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here