24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ahamasisha wawekezaji wa mafuta, sukari

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema  ili kukabiliana na upungufu wa sukari na mafuta ya kula nchini wawekezaji zaidi wanahitajika katika zao la kilimo cha michikichi na miwa.

Hayo aliyasema jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wataalamu wa kilimo na watafiti waliokutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya kukuza kilimo kitakachosaidia kuingia katika uchumi wa kati utakaopelekea uchumi wa viwanda nchini.

Alisema  tani  670,000 zinahitajika lakini uwezo wa uzalishaji ni tani 300,000 hivyo kuna upungufu wa tani 370,000 ambazo kama wawekezaji wataruhusiwa  na kulima miwa kwa wingi tatizo hilo litakua historia.

Pia alizungumzia  uhitaji wa mafuta ya kula ambapo alisema yanazalishwa  asilimia 36 na asilimia 64 yanaagizwa nje ya nchi na kufanya nchi kutumia mabilioni ya fedha.

Alisema anashangazwa na kuona nchi kama Malaysia inayonunua mbegu za michikichiki kutoka hapa nchini lakini wao wamekuwa wazalishaji wakubwa wa mafuta  kuliko wanapochukua mbegu.

Katika hatua nyingine Hasunga aliwataka maofisa ugani kusimamia wakulima ili pia wawasaidie katika kukuza uzalishaji na wahamasishe ili waache kulima kilimo cha mazoea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti Seliani cha mkoani Arusha, Dk. Joseph Nduguru, alisema mkutano huo utajadili mbinu mbalimbali za kuhakikisha mkulima anapata soko akiwa na mazao yaliyo bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles