28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Afrika Kusini aibua hoja ‘Xenophobia’

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amezitaka nchi za Afrika kudhibiti uhamiaji.

Kauli hiyo ya Pandor imekuja katika wakati ambao wimbi la mashambulizi dhidi ya wageni yaliyofanywa na raia wa Afrika Kusini likisababisha hasira.

Akizungumza na wawakilishi wa wahamiaji, pia alisema viongozi wa Afrika wasizifikishe nchi zao kwenye hali mbaya wakitarajia nchi nyingine kukabiliana na matokeo ya uhamiaji.

Watu 12 waliuawa mapema mwezi huu wakati kundi la watu lilipovamia na kushambulia wageni wanaoendesha biashara hususani katika jiji la Johannesburg.

Kati hao waathirika 10 walikuwa ni raia wa Afrika Kusini na wawili walikuwa ni Wazimbabwe.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wiki iliyopita alilazimika kuwaomba radhi waafrika  kutokana na kadhia hiyo.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa amesimama kwa ajili ya kutoa salamu ya rambirambi katika msiba wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe  alichukua hatua hiyo baada ya kuzomewa na umati wa watu waliokuwa wamekusanyika katika shughuli hiyo mjini Harare nchini Zambabwe.

Ramaphosa aliahidi umati huo kuendeleza kile walichosiamamia akina Mugabe na waasisi wengine wa ukombozi katika bara la Afrika akiwamo Nkame Nkruma wa Ghana ambao waliamini katika umoja.

Kiongozi huyo pia alilimbia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kuwa alijisikia aibu kutokana na mashambulizi hayo.

“Tumechukulia kwa uzito na kama taifa tumeiabishwa kwa sababu hili  linakwenda kinyume na kile ambacho Afrika Kusini inakisimamia,”  alisema.

Katika kutafuta ufumbuzi wa kadhia hiyo Pandor amependekeza kuwa suala la wahamiaji si tu la Afrika Kusini.

“Tunahitaji kuzungumza wajibu wa nchi nyingine kusaidia kama Afrika Kusini  Kenya, Uganda na nchi nyingine nyingi jinsi ya kudhibiti sawasawa suala la wahamiaji,” aliwaambia wajumbe wanaounda jukwaa la Diaspora.

Afrika Kusini imekuwa kama sumaku ya wahamiaji kutoka katika nchi nyingine za Afrika kutokana na hali yake nzuri ya uchumi na mazingira ya kufanya biashara.

Lakini bado inakabiliwa na kadhia kubwa ya  tatizo la ajira na baadhi ya wageni wanaona kuwa raia wa kigeni wanachukua nafasi yao.

Pandor amelitaka bara la Afrika  kuegukia maendeleo ya haraka ya kiuchumi kusaidia kukabiliana na idadi ya watu inayoongezeka.

” Hakuna kiongozi anayepaswa kuruhusiwa kuharibu taifa lake na kutarajia mtu mwingine abebe wajibu kwa watu wake,”  alisema.

Watu wanaohamia Afrika kusini ni kama maskini na wasio na ujuzi, kama ilivyo kwa mamilioni ya Waafrika  Kusini weusi “, Waziri huyo alikaririwa na BBC mapema wiki hii katika kipindi cha Hardtalk.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles